Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 33

33
Yakobo na Esau Wakutana
1 # Mwa 32:6 Yakobo akainua macho yake, akaona, na tazama, Esau anakuja na watu mia nne pamoja naye. Akawagawanyia Lea, na Raheli, na wale vijakazi wawili, wana wao. 2Akawaweka hao vijakazi na wana wao mbele, na Lea na wanawe nyuma yao, na Raheli na Yusufu mwisho. 3#Mwa 18:2; 42:6Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake. 4#Mwa 32:28; Mit 16:1; 21:1; Yer 10:23Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia. 5#Mwa 48:9; Zab 127:3; Isa 8:18Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake. 6Ndipo wale vijakazi, na wana wao, wakakaribia wakainama. 7Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama.
8 # Mwa 32:5,16 Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu. 9Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, uliyo nayo na yawe yako. 10#Mwa 43:3; 2 Sam 3:13; 14:24-32; Mt 18:10Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami. 11#Amu 1:15; 1 Sam 25:27; 2 Fal 5:15; Flp 4:18; 2 Fal 5:23Pokea, tafadhali, mbaraka wangu, ulioletewa, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote Akamshurutisha, naye akapokea.
12Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia. 13Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng’ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote. 14#Mwa 32:3Tafadhali bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri. 15#Rut 2:13Esau akasema, Nikuachie, basi, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana wangu. 16Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri. 17#Yos 13:27; Amu 8:5Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.
Yakobo Afika Shekemu
18 # Yn 3:23; Mdo 7:16; Yos 24:1 Yakobo akaja kwa amani mpaka mji wa Shekemu, ulio katika nchi ya Kanaani, alipokuja kutoka Padan-aramu; akapiga kambi mbele ya huo mji. 19#Yos 24:32; Yn 4:5; Mdo 7:16Akainunua sehemu ya nchi, alipopiga hema yake, kwa mkono wa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia vya fedha. 20#Mwa 35:7Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli.#33:20El-elohe-Israeli maana yake ni Mungu, Mungu wa Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

Mwa 33: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha