Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezr 2:64-70

Ezr 2:64-70 SUV

Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini, tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili. Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano; ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao elfu sita, na mia saba na ishirini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za baba zao, hapo walipoifikilia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu sitini na moja elfu, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia ya makuhani. Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.