Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 20

20
Amri Kumi za Mungu
1 # Kum 5:22 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2#Law 26:1; Kum 5:6; Zab 81:10; Hos 13:4; Kut 13:3Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3#Kum 6:14; 2 Fal 17:35; Yer 25:6Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 # Kut 34:17; Law 19:4; 26:1; Kum 4:15-18; 27:15 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5#Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kum 7:9-10; Yos 23:7; 24:19; 2 Fal 17:35; Isa 44:15; Nah 1:2; Isa 14:20; Yer 2:9; Eze 18:19Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6#Zab 89:34; Rum 11:28; Kum 7:9nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 # Law 19:12; Zab 15:4; Mt 5:33; Mik 6:11 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 # Kut 16:23-30; 31:12-14; Kum 5:12 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9#Kut 23:12; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Lk 13:14Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10#Mwa 2:2; Neh 13:16lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11#Mwa 2:1-3; Kut 31:17Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 # Kum 5:16; 27:16; Yer 35:7,8; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2-3; Law 19:3 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
13 # Mwa 9:6; Law 24:17; Mt 5:21; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11 Usiue.
14 # Law 20:10; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11 Usizini.
15 # Law 19:11; 1 The 4:6; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9 Usiibe.
16 # Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 # Rum 7:7; 13:9; Mik 2:2; Efe 5:3; Mit 6:29; Mt 5:28 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
18 # Ebr 12:18-19 Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. 19#Gal 3:19Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. 20#Mwa 22:1; Mit 3:7Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi. 21Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo.
Sheria Kuhusu Madhabahu
22BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni. 23Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie. 24#2 Nya 6:6; Mwa 12:2Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng’ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia. 25#Kum 27:5-7; Yos 8:31Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi. 26Tena hutapanda kwenda madhabahuni kwangu kwa daraja, uchi wako usidhihirike juu yake.

Iliyochaguliwa sasa

Kut 20: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia