Mhu 8
8
Mtii Mfalme na Ujifurahishe
1Ni nani aliye kama mwenye hekima;
Naye ni nani ajuaye kufasiri neno?
Hekima ya mtu humng’ariza uso wake,
Na ugumu wa uso wake hubadilika.
2 #
Rum 13:5
Mimi nasema hivi, Uishike amri ya mfalme; na hiyo kwa sababu umeapa kwa Mungu. 3Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo. 4#Ayu 34:18Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?
5Aishikaye amri hatajua neno baya;
Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu.
6 #
Mhu 3:1
Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa; 7#Mit 24:22; Mhu 6:12kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?
8 #
Zab 49:6; Ayu 14:5 Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho;
Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa;
Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile;
Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.
9 #
1 Sam 18:12
Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
Njia za Mungu Hazichunguziki
10Pia nikaona waovu wamezikwa, nao wamefika kaburini; tena waliofanya mema wameondoka katika patakatifu, nao wamesahauliwa mjini. Hayo nayo ni ubatili. 11#Ayu 21:14,15; Zab 10:6; Isa 26:10; Rum 2:4,5; 2 Pet 3:4,10Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya. 12#Isa 65:20; Rum 2:5; Mit 1:32; Isa 3:10; Mt 25:34Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake; 13walakini haitakuwa heri kwa mwovu, wala hatazidisha siku zake, zilizo kama kivuli; kwa sababu hana kicho mbele za Mungu.
14 #
Zab 73:14; Mhu 2:14 Kuna ubatili unaofanyika juu ya nchi, kwamba wako wenye haki nao wapatilizwa kama kwa kazi yao waovu; tena wako waovu, nao wapatilizwa kama kwa kazi yao wenye haki. Nami nikasema ya kuwa hayo nayo ni ubatili. 15#Mhu 3:12; Law 26:5Kisha nikaisifu furaha, kwa sababu mwanadamu hana neno lo lote lililo jema chini ya jua, kuliko kula, na kunywa, na kucheka; na yakuwa hilo likae naye katika amali yake, siku zote za maisha yake alizompa Mungu chini ya jua.
16Mimi nilipotia moyo wangu katika kuijua hekima, na kuuona utumishi uliofanyika juu ya nchi, (maana kuna asiyepata usingizi kwa macho yake mchana wala usiku); 17#Ayu 5:9; Mhu 3:11; Isa 40:28; Rum 11:33; Zab 73:16basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.
Iliyochaguliwa sasa
Mhu 8: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.