Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kum 34

34
Kifo cha Musa na Kuzikwa kwake katika Moabu
1 # Yos 19:40-48; Amu 18:28 Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. BWANA akamwonyesha nchi yote ya Gileadi hata Dani; 2#Kut 23:31; Hes 34:6; Kum 11:24; Yos 15:12na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi; 3#Amu 1:16; 3:13; 2 Nya 28:15na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari. 4#Mwa 12:7; 26:3; 28:13BWANA akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko. 5#Kum 32:50; Yos 1:1,2; Mal 4:4Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la BWANA. 6#Yud 1:9Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo. 7#Kum 31:2; Mwa 27:1; 48:10; Yos 14:10Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka. 8#Mwa 50:3; Hes 20:29; 1 Sam 25:1; Isa 57:1; Mdo 8:2Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha. 9#Kut 31:3; Hes 11:17; 1 Fal 9:12; Isa 11:2; Dan 6:3; Hes 27:18Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama BWANA alivyomwamuru Musa. 10#Kut 33:11; Kum 18:15,18; Hes 12:6; Kum 5:4Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso; 11katika ishara zote na maajabu yote, ambayo BWANA alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; 12na katika ule mkono wa nguvu wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote.

Iliyochaguliwa sasa

Kum 34: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia