Amo 2
2
1 #
Isa 15:1—16:14; 25:10-12; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa; Sef 2:8-11; 2 Fal 3:27 2#Yer 48:41lakini nitapeleka moto juu ya Moabu, nao utayateketeza majumba ya Keriothi; na Moabu atakufa pamoja na mshindo, na kelele, na sauti ya tarumbeta; 3#Hes 24:17; Yer 48:7nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA.
Hukumu kwa Yuda
4 #
Law 26:14; 2 Sam 12:9,10; 2 Nya 36:14-17; Neh 1:7; Isa 5:24; 28:15; Eze 20:13,16; Dan 9:11; Yer 16:19 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata; 5#Hos 8:14lakini nitapeleka moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu.
6 #
Isa 29:21; Amo 5:11,12 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu; 7#Isa 10:2; Eze 22:11; Law 20:3; Eze 36:20; Rum 2:24nao hutwetea mavumbi yaliyo juu ya vichwa vya maskini, na kuipotosha njia ya mwenye upole; na mtu na baba yake humwendea mwanamke mmoja, hata kulitia unajisi jina langu takatifu; 8#Kut 22:26; 1 Kor 10:21nao hujilaza karibu na kila madhabahu juu ya nguo zilizowekwa rehani, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya watu waliotozwa fedha. 9#Hes 21:24; Kum 3:8-11Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini. 10Pia naliwapandisha ninyi kutoka nchi ya Misri, nikawaongoza muda wa miaka arobaini jangwani, ili mpate kuimiliki nchi ya Mwamori. 11#Amu 13:5; Hes 6:1-8Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema BWANA. 12#Isa 30:10; Mdo 4:18Lakini mliwapa Wanadhiri mvinyo wanywe; mkawaamuru manabii, mkisema, Msifanye unabii.
13Tazameni, nitawalemea ninyi,
Kama gari lilemeavyo lililojaa miganda.
14Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio;
Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake;
Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
15Wala apindaye upinde hatasimama;
Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka;
Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake;
16Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa
Atakimbia uchi siku ile, asema BWANA.
Iliyochaguliwa sasa
Amo 2: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.