Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 The 3

3
Hitaji la Maombi
1 # Kol 4:3; 1 The 5:25 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; 2tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani. 3#1 The 5:24Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. 4#1 The 4:10; Gal 5:10; 2 Kor 7:16Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya. 5Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
Onyo juu ya Kutofanya Kazi
6 # Mt 18:17; Rum 16:17; 1 The 5:14; 4:1 Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu. 7#1 The 2:1; 1:6Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu; 8#1 Kor 4:12; Flp 3:17; 1 The 2:9wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. 9#Mt 10:10; 1 Kor 4:16; 1 The 1:6,7Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate. 10#Mwa 3:19; 1 The 3:4; 4:11Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. 11#1 The 5:14Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. 12#1 The 4:11Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe. 13#Gal 6:9Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema. 14#1 Kor 5:9,11Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari; 15#1 The 5:13,14lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
Salamu za Mwisho na Baraka
16 # 1 The 5:23 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
17 # 1 Kor 16:21 Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.

Iliyochaguliwa sasa

2 The 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia