2 Sam 23
23
Maneno ya Mwisho ya Daudi
1Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi.
Daudi, mwana wa Yese, anena,
Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu,
Yeye, masihi#23:1 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam. 2:10). wake Mungu wa Yakobo,
Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;
2 #
2 Pet 1:21
Roho ya BWANA ilinena ndani yangu,
Na neno lake likawa ulimini mwangu.
3 #
Kut 18:21
Mungu wa Israeli alisema,
Mwamba wa Israeli aliniambia,
Atawalaye wanadamu kwa haki,
Akitawala katika kicho cha Mungu,
4 #
Mit 4:18
Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo,
Asubuhi isiyo na mawingu.
Lachipuza majani mabichi juu ya nchi,
Kwa mwangaza baada ya mvua;
5 #
1 Fal 9:4-6
Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA?
Kwa kuwa amefanya nami agano la milele;
Ina taratibu katika yote, ni thabiti,
Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.
6Lakini hatawachipuza watu wa ubatili;
Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa,
Ambayo haivuniki kwa mkono,
7Mtu atakayeigusa hiyo,
Na awe na chuma na mpini wa mkuki,
Nao watateketezwa papo hapo kwa moto.
Mashujaa wa Daudi
8Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu#23:8 Au, Yosheb-bashebethi. Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja. 9#1 Nya 11:12; 27:4Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; 10huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. 11#1 Nya 11:12Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; 12ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
13 #
1 Nya 11:15; 14:9; Kum 33:29; 1 Sam 22:1; 1 Nya 29:11; 2 Nya 14:11-14; 25:8; Zab 3:8; 46:1; Mit 21:30,31; Rum 8:31; 2 Sam 5:18; Isa 17:5 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. 14#1 Sam 22:4; 1 Nya 12:16Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu. 15Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 16Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA. 17#Law 17:10Akasema, Hasha, BWANA, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
18 #
2 Sam 2:18; 1 Nya 11:20 Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu. 19Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. 20#Yos 15:21; Kut 15:15Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu,#23:20 Au, wana wawili wa Arieli, wa Moabu. pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji; 21#1 Nya 11:23huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. 22Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. 23#2 Sam 8:18Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.
24 #
2 Sam 2:18
Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu; 25#1 Nya 11:27na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi; 26na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; 27na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi; 28na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi; 29na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini; 30#Amu 12:15; 2:9na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi; 31na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi; 32na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani, 33mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari; 34na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni; 35na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi; 36na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi; 37na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; 38#2 Sam 20:26; Yos 15:48na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri; 39#2 Sam 11:3,6na Uria, Mhiti; jumla yao ilikuwa watu thelathini na saba.
Iliyochaguliwa sasa
2 Sam 23: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.