Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 31

31
Madhabahu za Kipagani Zaharibiwa
1 # 2 Fal 18:4; 2 Nya 13:14 Basi hayo yote yalipokwisha, wakatoka Israeli wote waliokuwako waende miji ya Yuda, wakazivunja-vunja nguzo, wakayakata-kata maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hata walipokwisha kuviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao. 2#1 Nya 23:6,30,31Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa matuo ya BWANA. 3#Hes 28:1; 29:1Tena akaweka sehemu ya mfalme ya mali zake kwa sadaka za kuteketezwa, yaani, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa za sabato, na za mwezi mpya, na sikukuu, kama ilivyoandikwa katika torati ya BWANA. 4#Hes 18:8; Neh 13:10; 1 Kor 9:13; Mal 2:7Tena akawaamuru watu waliokaa Yerusalemu, watoe sehemu ya makuhani na Walawi, ili hao wajibidiishe katika torati ya BWANA. 5#Kut 22:29; 23:19; Law 25:23; Hes 18:12; Neh 13:12; Mit 3:9; Eze 20:40; 44:30; 1 Kor 15:20; Yak 1:18Mara ilipotangaa amri, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, na divai, na mafuta, na asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta nyingi. 6#Law 27:30; Kum 14:28Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng’ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa BWANA, Mungu wao, wakaviweka chungu chungu. 7Katika mwezi wa tatu wakaanza kuweka misingi ya hizo chungu, wakazimaliza katika mwezi wa saba. 8#Mwa 14:19; Kum 33:29; 2 Sam 6:18; 1 Fal 8:55,56; 2 Nya 6:3; Zab 33:12; 144:15Hata walipokuja Hezekia na wakuu, na kuziona zile chungu, wakamhimidi BWANA, na watu wake Israeli. 9Ndipo Hezekia akaulizana na makuhani na Walawi katika habari ya hizo chungu. 10#Hag 2:19; Mal 3:10Azaria kuhani mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa BWANA, tumekula na kushiba, na kusaza tele; kwa kuwa BWANA amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa.
Utaratibu wa Makuhani na Walawi Wapangwa Upya
11Ndipo Hezekia akaamuru kutengeneza vyumba nyumbani mwa BWANA; wakavitengeneza. 12#Neh 13:13Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; na juu yake Konania Mlawi alikuwa mkuu, na wa pili ni Shimei nduguye. 13Na Yehieli, na Azaria, na Nahathi, na Asaheli, na Yerimothi, na Yozabadi, na Elieli, na Ismakia, na Mahathi, na Benaya, walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei nduguye, kwa amri ya Hezekia mfalme, na Azaria mkuu wa nyumba ya Mungu. 14Na Kore, mwana wa Imna, Mlawi, bawabu wa mlango wa mashariki, alizisimamia sadaka za hiari za Mungu; ili kugawa matoleo ya BWANA, navyo vitu vilivyokuwa vitakatifu sana. 15#Yos 21:9; 1 Nya 9:22Na chini yake walikuwa Edeni, na Minyamini, na Yeshua, na Shemaya, na Amaria, na Shekania, mijini mwa makuhani, kwa walivyoaminiwa, ili kuwagawia ndugu zao kwa zamu, wakuu na wadogo sawasawa; 16zaidi ya wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wanaume, wenye miaka mitatu na zaidi, kila mmoja aliyeingia nyumbani mwa BWANA, kama ilivyopasa kazi ya kila siku, kwa huduma zao katika malinzi yao, kwa kadiri ya zamu zao; 17#1 Nya 23:24,27na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya makuhani kufuata nyumba za baba zao, na Walawi, wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, katika malinzi yao, kwa kadiri ya zamu zao; 18na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wadogo wao wote, wake zao, na wana wao, na binti zao, katika kusanyiko lote; kwani kwa vile walivyoaminiwa, wakajitakasa katika utakatifu; 19#Law 25:34; Hes 35:2; 2 Nya 31:12-15tena kwa ajili ya wana wa Haruni makuhani, waliokuwamo mashambani mwa malisho ya miji yao, mji kwa mji, kulikuwa na watu waliotajwa majina yao, ili kuwagawia sehemu wanaume wote miongoni mwa makuhani, na wote waliohesabiwa kwa nasaba miongoni mwa Walawi. 20#1 Fal 15:5; 2 Fal 20:3; 22:2; Yn 1:47; 1 The 2:10Na hivyo ndivyo alivyofanya Hezekia katika Yuda yote; akatenda yaliyo mema, na ya adili, na uaminifu, mbele za BWANA, Mungu wake. 21#Kum 29:9; Yos 4:7; Zab 1:3; Mit 3:9; Mal 3:10; 1 Tim 4:8Na katika kila kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, na kwa torati, na kwa amri, ili kumtafuta Mungu wake, aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 31: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha