Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 24

24
Yoashi Atengeneza Hekalu
1 # 2 Fal 11:21; 12:1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala miaka arobaini huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Sibia wa Beer-sheba. 2#2 Nya 25:2; 26:5Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote za Yehoyada kuhani. 3Yehoyada akamwoza wake wawili, naye akazaa wana na binti. 4Ikawa baada ya haya, Yoashi alikuwa na nia ya kuitengeneza nyumba ya Mungu. 5#2 Fal 12:4; 2 Nya 29:3; 34:8Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni mijini mwa Yuda, mkakusanye katika Israeli wote fedha, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Walakini Walawi hawakuliharakisha. 6#2 Fal 12:7; Kut 30:12-16; Hes 1:50; 17:7,8; Mdo 7:44Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda? 7#2 Nya 21:17; 22:3,4; Zab 12:8; 2 Fal 12:4Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia mabaali. 8#2 Fal 12:9Basi mfalme akaamuru, nao wakafanyiza kasha, wakaliweka nje langoni pa nyumba ya BWANA. 9#Kut 36:6Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea BWANA kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani. 10Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata wakaisha. 11#2 Fal 12:10Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele. 12Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA. 13#Neh 4:7Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara. 14#1 Fal 7:50; 2 Fal 12:13; Kut 29:38; Ebr 7:27; 1 Pet 1:18,19; Ufu 5:9Nao walipokwisha, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, vikafanyizwa kwayo vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, daima, siku zote za Yehoyada.
15 # Ayu 5:26 Lakini Yehoyada akawa mzee, mwenye umri mwingi, akafa; alipokufa alikuwa na umri wa miaka mia na thelathini. 16#1 Fal 2:10Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake. 17#Mdo 20:29Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao. 18#1 Fal 14:23; Yos 22:20; Amu 5:8; 2 Sam 24:1; 2 Nya 19:2; 28:13; Hos 5:10Wakaiacha nyumba ya BWANA, Mungu wa baba zao; wakatumikia maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao. 19#2 Nya 36:15; Neh 9:26; Yer 7:25,26; 25:4; Lk 11:47-51Hata hivyo akawapelekea manabii, ili kuwarudisha kwa BWANA; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza. 20#2 Nya 15:1,2; Amu 6:34; Hes 14:41; 1 Sam 13:13,14; Kum 29:25,26; Yer 2:19Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi. 21#Mt 23:35; Mdo 7:58Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya BWANA. 22Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayatakie kisasi.
Kifo cha Yoashi
23 # 2 Fal 12:17 Ikawa mwisho wa mwaka, wakakwea juu yake jeshi la Washami; wakafika Yuda na Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wa watu wote miongoni mwa watu, wakamletea mfalme wa Dameski nyara zao zote. 24#Law 26:8,25; Kum 32:30; Isa 30:17; Kum 28:25; Isa 10:5Maana wakaja jeshi la Washami watu haba; BWANA akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao. Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu. 25#2 Fal 12:18,20; Zab 10:14Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme. 26Na hawa ndio waliomfanyia fitina, Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi. 27Basi kwa habari ya wanawe, na ukubwa wa mizigo aliolemewa, na majengo ya nyumba ya Mungu, tazama, hayo yameandikwa katika maelezo ya kitabu cha wafalme. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 24: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia