Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 14

14
Asa Atawala
1 # 1 Fal 15:8 Basi Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi, akatawala Asa mwanawe mahali pake; katika siku zake nchi ikastarehe miaka kumi.
2Basi, Asa akafanya yaliyo mema, yaliyo ya adili, machoni pa BWANA, Mungu wake; 3#1 Fal 15:14; 2 Nya 15:17; Kut 34:13; 1 Fal 11:7maana aliziondoa madhabahu za kigeni, na mahali pa juu, akazivunja nguzo, akayakata-kata maashera; 4akawaamuru Yuda wamtafute BWANA, Mungu wa baba zao, na kuzitenda torati na amri. 5Tena akaondoa kutoka miji yote ya Yuda mahali pa juu na sanamu za jua; ufalme ukastarehe mbele yake. 6Akajenga miji yenye maboma katika Yuda; kwa kuwa nchi ilikuwa imestarehe, wala hakuwa na vita miaka ile; kwa sababu BWANA amemstarehesha. 7Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta BWANA, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa. 8Naye Asa alikuwa na jeshi waliochukua ngao na mikuki, katika Yuda mia tatu elfu; na katika Benyamini wenye kuchukua vigao na kupinda upinde, mia mbili na themanini elfu; hao wote walikuwa mashujaa.
Uvamizi wa Kushi Wazimwa
9 # 2 Nya 16:8; Yos 15:44; Mik 1:15 Kisha, akatoka juu yao Zera Mkushi, mwenye jeshi elfu elfu, na magari mia tatu; akaja Maresha. 10Akatoka Asa amlaki, wakapanga vita Maresha bondeni mwa Sefatha. 11#Kut 14:10; 1 Nya 5:20; 2 Nya 13:14; Zab 22:5; Mdo 2:21; Amu 7:7; 1 Sam 14:6; 2 Kor 12:9,10; 1 Sam 17:45; Mit 18:10; Nah 1:7Naye Asa akamlilia BWANA, Mungu wake, akasema, BWANA, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee BWANA, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu. 12#2 Nya 13:15Basi, BWANA akawapiga Wakushi mbele ya Asa, na mbele ya Yuda; na Wakushi wakakimbia. 13#Mwa 10:19; 20:1; Zab 46:1-11Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; nao wengi wakaanguka wa Wakushi hata wasiweze kupona; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka mengi sana. 14#Mwa 35:5; Kut 15:16; Kum 11:25; 2 Nya 17:10; 20:29Wakaipiga miji yote kando-kando ya Gerari; maana hofu ya BWANA ikawajia; nao wakaiteka nyara miji yote, kwa maana zilikuwamo ndani yake nyara nyingi mno. 15Wakazipiga pia hema za ng’ombe, wakachukua kondoo wengi na ngamia, wakarudi Yerusalemu.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 14: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia