Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Fal 21

21
Shamba la Nabothi
1 # Amu 6:33; 1 Sam 29:1 Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria. 2#Mwa 3:6; Kut 20:17; Kum 5:21; Hab 2:9; Lk 12:15; 1 Tim 6:9,10; Yak 1:14,15; 1 Yoh 2:16; 1 Sam 8:14Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake. 3#Law 25:23; Hes 36:7; Eze 46:18Nabothi akamwambia Ahabu, BWANA apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu. 4Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula.
5Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula? 6Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu. 7#1 Sam 8:14; Yer 6:7; Mik 2:1; 7:3Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli. 8Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi. 9Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu, 10#Kum 13:13; Amu 19:22; 1 Sam 2:12; 2 Sam 20:1; 23:6; 2 Kor 6:15; Kut 22:28; Law 24:15,16; Mdo 6:11; Law 24:14mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe. 11Wale wazee wa mji wake, na walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea. 12#Ayu 15:34; 34:30; Mit 11:9; 29:12; Isa 9:16,17; 32:6,7; 1 Tim 4:2Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu. 13#Hes 15:36; Yos 7:24; 2 Nya 24:21; Mk 15:20; Mdo 7:58,59; Ebr 11:37Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa. 14Wakampelekea Yezebeli habari, wakasema, Nabothi amepigwa kwa mawe, amekufa. 15Ikawa Yezebeli aliposikia ya kwamba Nabothi amepigwa kwa mawe na kufa, Yezebeli akamwambia Ahabu, Inuka, ulitamalaki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, alilokataa kukupa kwa fedha, maana Nabothi hako hai, lakini amekufa. 16Ikawa Ahabu aliposikia ya kwamba Nabothi amekufa, akaondoka, alitelemkie shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ili alitamalaki.
Eliya Atangaza Hukumu ya Mungu
17 # Zab 9:12 Neno la BWANA likamjia Eliya Mtishbi, kusema, 18#1 Fal 13:32; 2 Nya 22:9Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, akaaye katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. 19#Mwa 4:9-11; 2 Sam 12:9; 1 Fal 22:38Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako. 20#1 Fal 18:17; Isa 29:21; Amo 5:10; 2 Fal 17:17; Rum 7:14Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa BWANA. 21#1 Fal 14:10; Kum 32:35; 2 Fal 9:8; Zab 94:1-23; 1 Sam 25:22Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli. 22#1 Fal 15:29; 16:3,11Kisha nitaifanya nyumba yako iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata kunighadhibisha, ukawakosesha Israeli. 23#2 Fal 9:36; Zab 7:16; 9:15,16Tena BWANA alinena habari za Yezebeli, akisema, Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli. 24#1 Fal 14:11; 16:4Mtu wa nyumba ya Ahabu afaye mjini, mbwa watamla, na yeye afaye mashambani ndege wa angani watamla.
25 # 1 Fal 16:30,31; 11:1,4; Mwa 6:2-5 (Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa BWANA ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. 26#Mwa 15:16; 2 Fal 21:11Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)
27 # Mwa 37:34 Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole. 28Neno la BWANA likaja kwa Eliya Mtishbi, kusema, 29#Zab 66:20; 78:34-37; 2 Fal 9:25Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.

Iliyochaguliwa sasa

1 Fal 21: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia