1 Nya 8
8
Wazawa wa Benyamini
1 #
Mwa 46:21; Hes 26:38; 1 Nya 7:6 Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu; 2na wa nne Noha, na wa tano Rafa. 3Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi; 4na Abishua, na Naamani, na Ahoa; 5na Gera, na Shufamu, na Huramu. 6#1 Nya 2:52Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi; 7na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi. 8#Rut 1:1Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara. 9Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu; 10na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao. 11Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali. 12#Ezr 2:33; Neh 6:2Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake; 13#Yos 19:42na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi. 14Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi; 15na Zebadia, na Aradi, na Ederi; 16na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria. 17Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi; 18na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali. 19Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi; 20na Elienai, na Silethai, na Elieli; 21na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema. 22Na Ishpani, na Eberi, na Elieli; 23na Abdoni, na Zikri, na Hanani; 24na Hanania, na Elamu, na Anthothiya; 25na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki. 26Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia; 27na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu. 28Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu.
29 #
1 Nya 9:35
Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka; 30na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali,#8:30 Taz. 1 Nyakati 9:36. na Nadabu; 31#1 Nya 9:37na Gedori, na Ahio, na Zekaria#8:31 Taz. 1 Nyakati 9:37., 32Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao. 33#1 Sam 9:1; 14:51; 1 Nya 9:36,39; Mdo 13:21; 2 Sam 2:8Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali. 34#2 Sam 4:4; 9:12Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika. 35#1 Nya 9:41Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi. 36Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa; 37na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli; 38naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli. 39Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti. 40#1 Nya 12:2; 2 Nya 11:1; 13:3; Neh 4:13; Wim 3:7,8; Efe 6:11-20Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.
Iliyochaguliwa sasa
1 Nya 8: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.