1 Nya 6
6
Wazawa wa Lawi
1 #
Mwa 46:11
Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. 2Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. 3#Kut 6:23; 24:1; Law 10:1Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 4Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua; 5na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi; 6na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi, 7na Merayothi akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu; 8#2 Sam 8:17; 15:27na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Ahimaasi; 9na Ahimaasi akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Yohana; 10#2 Nya 26:17,18; 1 Fal 6:1; 2 Nya 3:1na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu) 11#Ezr 7:3na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu; 12na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu; 13na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria; 14#Neh 11:11na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki; 15#2 Fal 25:18; 2 Nya 36:17-21na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.#6:15 Au, Nebukadneza.
16 #
Kut 6:16
Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. 17Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei. 18Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. 19#Hes 3:33; 1 Nya 23:21Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao. 20Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima; 21#1 Nya 6:41,42na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai. 22Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri; 23na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri; 24na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli. 25Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi. 26Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu; 27na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana. 28Na wana wa Samweli; Yoeli, mzaliwa wa kwanza, na wa pili Abia. 29Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza; 30na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.
Waimbaji Walioteuliwa na Daudi
31 #
1 Nya 16:1; 2 Sam 6:17; 1 Fal 8:4 Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe. 32Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao. 33Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli; 34mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu; 35mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai; 36mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli; 37#Kut 6:24mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; 38mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli. 39Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea; 40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya; 41mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido; 42mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei; 43mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. 44Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki; 45mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia; 46mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri; 47mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. 48Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu.
49 #
Kut 29:38; 30:1; Law 1:9; 10:19,20; Hes 3:10; 18:7; Ebr 5:1; Kut 30:7; 1 Sam 2:28; 1 Nya 23:13; Lk 1:9 Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu. 50#Kut 6:23; Law 10:1; Hes 3:2; 26:60; 1 Nya 24:1; Ezr 7:2-5Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua; 51na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia; 52na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu; 53na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi.
Makao ya Walawi
54 #
Hes 35:1-9; Yos 21:9-19 Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza; 55#Yos 21:11,12wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka; 56#Yos 14:13; 15:13bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune. 57#Yos 21:13Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake; 58#Yos 21:15na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake; 59#Yos 21:16na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake; 60#Yos 21:18tena katika kabila ya Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu. 61#Yos 21:5Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hiyo, yaani, nusu-kabila, nusu ya Manase. 62Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani. 63#Yos 21:7,34Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni. 64#Hes 35:1-8; Yos 21:41,42Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake. 65Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, na katika kabila ya wana wa Benyamini. 66#Yos 21:4-26Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila ya Efraimu. 67#Mwa 33:19; Yos 21:21Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake; 68na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake; 69na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake; 70na katika nusu-kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi. 71#Yos 21:27; Kum 1:4Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake; 72na katika kabila ya Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake; 73na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake; 74na katika kabila ya Asheri; Mishali pamoja na viunga vyake, na Abdoni pamoja na viunga vyake; 75na Helkathi pamoja na viunga vyake, na Rehobu pamoja na viunga vyake; 76na katika kabila ya Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake. 77Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila ya Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake; 78na ng’ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila ya Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake, 79na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake; 80na katika kabila ya Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake; 81#Hes 21:25; Kum 2:24; Yos 13:10; Isa 15:4; Yer 48:34na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake.
Iliyochaguliwa sasa
1 Nya 6: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.