1 Nya 4
4
Wazawa wa Yuda
1 #
Mwa 38:29; 46:12; Hes 26:20,21; Rut 4:18 Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali. 2Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi. 3Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na umbu lao aliitwa jina lake Haselelponi; 4na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, babaye Bethlehemu. 5Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. 6Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara. 7Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani. 8Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu. 9#Mwa 34:19; Zab 112:6; Mit 10:7; Mwa 3:16Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 10#Mwa 12:8; 1 Nya 16:8; Ayu 12:4; 22:27; Isa 12:4; 1 Fal 3:7-13; Zab 21:4; 65:2; Mt 7:7-11Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
11Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni. 12Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka. 13#Yos 15:17Na wana wa Kenazi; Othnieli, na Seraya; na wana wa Othnieli; Hathathi. 14#Neh 11:35Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye bonde la Wakarashi; kwani hao walikuwa mafundi. 15Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi. 16Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli. 17Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa. 18Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa. 19Na wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka. 20Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.
21 #
Mwa 38:1
Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa mbari ya wafuma nguo za kitani safi, wa mbari ya Ashbea; 22#2 Sam 8:2na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. Na taarifa hizi ni za zamani sana. 23Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.
Wazawa wa Simeoni
24Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli; 25na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma. 26Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei. 27Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda. 28Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali; 29na huko Bilha, na Esemu, na Toladi; 30na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi; 31na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hata wakati wa kumiliki Daudi. 32Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano, 33na vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo. 34Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia; 35na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli; 36na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya; 37na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya; 38hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na mbari za baba zao zikaongezeka sana. 39Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo zao malisho. 40#Mwa 9:22; 10:6; Zab 78:51Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa na nafasi, tena imetulia, na kuwa na amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu. 41#2 Fal 18:8Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuzipiga hema zao, pamoja na hao Wameuni walioonekana huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo zao. 42Na baadhi yao, maana ya hao wana wa Simeoni, watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi. 43#1 Sam 15:8; 30:17; 2 Sam 8:12Nao wakawapiga mabaki ya Waamaleki waliookoka, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.
Iliyochaguliwa sasa
1 Nya 4: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.