Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Sefania 3:14-17

Sefania 3:14-17 NEN

Imba, ee Binti Sayuni; paza sauti, ee Israeli! Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee Binti Yerusalemu! BWANA amekuondolea adhabu yako, amewarudisha nyuma adui zako. BWANA, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe; kamwe hutaogopa tena madhara yoyote. Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu, “Usiogope, ee Sayuni; usiiache mikono yako ilegee. BWANA Mungu wako yu pamoja nawe, yeye ni mwenye nguvu kuokoa. Atakufurahia kwa furaha kubwa, atakutuliza kwa pendo lake, atakufurahia kwa kuimba.”