Zaburi 73:21-28
Zaburi 73:21-28 NENO
Moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu, nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume. Unaniongoza kwa ushauri wako, hatimaye utaniingiza katika utukufu. Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele. Wale walio mbali nawe wataangamia, unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako. Lakini kwangu mimi, ni vyema kuwa karibu na Mungu. Nimemfanya Bwana Mungu Mwenyezi kimbilio langu; nami nitayasimulia matendo yako yote.