Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 38:1-10

Zaburi 38:1-10 NEN

Ee BWANA, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia. Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika. Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. Ee BWANA, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza.