Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 139:7-12

Zaburi 139:7-12 NEN

Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko. Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, kama nikikaa pande za mbali za bahari, hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 139:7-12