Zaburi 119:97-104
Zaburi 119:97-104 NENO
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa. Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima. Nina akili kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako. Nina ufahamu kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako. Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako. Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu! Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.