Mithali 24:1-6
Mithali 24:1-6 NEN
Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara. Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu, kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi.