Hesabu 29
29
Sikukuu ya Tarumbeta
(Walawi 23:23-25)
1“ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. 2Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayo Mwenyezi Mungu ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 3Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu mbili za kumi ya efa; 4na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga. 5Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 6Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku, pamoja na sadaka zake za nafaka, na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, harufu inayopendeza.
Siku ya Upatanisho
(Walawi 23:26-32)
7“ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi. 8Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu. 9Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini; 10na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja. 11Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.
Sikukuu ya Vibanda
(Walawi 23:33-44)
12“ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwa Mwenyezi Mungu kwa siku saba. 13Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu. 14Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini; 15na kwa wana-kondoo kumi na wanne, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi ya efa ya unga laini. 16Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka yake ya kinywaji.
17“ ‘Katika siku ya pili, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 18Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 19Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zake za vinywaji.
20“ ‘Katika siku ya tatu, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 21Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 22Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
23“ ‘Katika siku ya nne, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 24Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 25Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
26“ ‘Katika siku ya tano, andaeni mafahali tisa, kondoo dume wawili na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 27Pamoja na mafahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za kinywaji kulingana na idadi iliyoainishwa. 28Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
29“ ‘Katika siku ya sita, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 30Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 31Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
32“ ‘Katika siku ya saba, andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 33Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 34Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
35“ ‘Katika siku ya nane, mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida. 36Toeni sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri inayompendeza Mwenyezi Mungu, sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 37Pamoja na fahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka, na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 38Ongeza beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
39“ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwenye sikukuu zenu zilizoamriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”
40Musa akawaambia Waisraeli yale yote Mwenyezi Mungu alimwagiza.
Iliyochaguliwa sasa
Hesabu 29: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.