Hesabu 27:18-20
Hesabu 27:18-20 NENO
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho wa Mungu yuko ndani yake, uweke mkono juu yake. Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao. Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli wapate kumtii.