Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 8:30-33

Marko 8:30-33 NEN

Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake. Ndipo akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa Mwana wa Adamu lazima atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini baada ya siku tatu afufuke. Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea. Lakini Yesu alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Marko 8:30-33