Marko 3:14-20
Marko 3:14-20 NEN
Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro); Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu. Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula.