Mathayo 27:57, 58, 59, 60, 61, 62, 63, 64, 65
Mathayo 27:57 NENO
Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Isa.
Mathayo 27:58 NENO
Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Isa. Pilato akaamuru apewe.
Mathayo 27:59 NENO
Yusufu akauchukua mwili wa Isa, akaufunga kwa kitambaa cha kitani safi
Mathayo 27:60 NENO
na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake.
Mathayo 27:61 NENO
Mariamu Magdalene na yule Mariamu mwingine walikuwa mahali pale, wakiwa wameketi mkabala na kaburi.
Mathayo 27:62 NENO
Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakamwendea Pilato
Mathayo 27:63 NENO
na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu wakati alikuwa bado hai alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’
Mathayo 27:64 NENO
Basi uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti hadi baada ya siku tatu. La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”
Mathayo 27:65 NENO
Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari walinzi. Nendeni, liwekeeni ulinzi kadiri mnavyoweza.”