YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo 23:29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37, 38

Mathayo 23:29 NENO

“Ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.

Mathayo 23:30 NENO

Nanyi mwasema, ‘Kama tungeishi wakati wa baba zetu, hatungeshiriki katika kumwaga damu ya manabii!’

Mathayo 23:31 NENO

Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii.

Mathayo 23:32 NENO

Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu!

Mathayo 23:33 NENO

“Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya Jehanamu?

Mathayo 23:34 NENO

Kwa sababu hii, tazameni, natuma kwenu manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine.

Mathayo 23:35 NENO

Hivyo ile damu ya wenye haki wote iliyomwagwa hapa duniani, tangu damu ya Habili, aliyekuwa mwenye haki, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemuua kati ya patakatifu na madhabahu, itawajia juu yenu.

Mathayo 23:36 NENO

Amin, nawaambia, haya yote yatakuja kwa kizazi hiki.

Mathayo 23:37 NENO

“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!

Mathayo 23:38 NENO

Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa.