Mathayo 16:1, 2, 3, 4
Mathayo 16:1 NENO
Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Isa na kumjaribu kwa kumwomba awaoneshe ishara kutoka mbinguni.
Mathayo 16:2 NENO
Isa akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’
Mathayo 16:3 NENO
Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua ishara za nyakati.
Mathayo 16:4 NENO
Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Isa akawaacha, akaenda zake.