YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo 11:25, 26, 27, 28, 29

Mathayo 11:25 NENO

Wakati huo Isa alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo.

Mathayo 11:26 NENO

Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

Mathayo 11:27 NENO

“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.

Mathayo 11:28 NENO

“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Mathayo 11:29 NENO

Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu.