YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo 1:18, 19, 20, 21, 22, 23, 24

Mathayo 1:18 NENO

Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Mathayo 1:19 NENO

Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, hivyo basi alikusudia kumwacha kwa siri.

Mathayo 1:20 NENO

Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Mathayo 1:21 NENO

Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Yesu, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

Mathayo 1:22 NENO

Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilonena kupitia nabii, aliposema

Mathayo 1:23 NENO

“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli” (maana yake, “Mungu pamoja nasi”).

Mathayo 1:24 NENO

Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya jinsi alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Mariamu kuwa mke wake.