Luka 9:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8
Luka 9:1 NENO
Isa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote
Luka 9:2 NENO
kisha akawatuma waende wakahubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
Luka 9:3 NENO
Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.
Luka 9:4 NENO
Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
Luka 9:5 NENO
Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Luka 9:6 NENO
Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.
Luka 9:7 NENO
Basi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yahya amefufuliwa kutoka kwa wafu.
Luka 9:8 NENO
Wengine wakasema Ilya amewatokea, na wengine kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka.