YouVersion Logo
Search Icon

Luka 9:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8

Luka 9:1 NEN

Yesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote

Luka 9:2 NEN

kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.

Luka 9:3 NEN

Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.

Luka 9:4 NEN

Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.

Luka 9:5 NEN

Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”

Luka 9:6 NEN

Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Luka 9:7 NEN

Basi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu.

Luka 9:8 NEN

Wengine wakasema Eliya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka.