Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 7:1-6, 8-10

Luka 7:1-6 NENO

Baada ya Isa kumaliza kusema haya yote kwa watu waliokuwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu. Mtumishi wa jemadari mmoja Mrumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu na kufa. Jemadari huyo aliposikia habari za Isa, aliwatuma wazee wa Wayahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari. Wale wazee walipofika kwa Isa, wakamsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili wewe umfanyie jambo hili, kwa sababu analipenda taifa letu tena ametujengea sinagogi.” Hivyo Isa akaongozana nao. Lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani, yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia Isa, “Bwana, usijisumbue, kwani mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu.

Luka 7:8-10 NENO

Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.” Isa aliposikia maneno haya, alishangazwa naye sana. Akageukia umati ule wa watu waliokuwa wanamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.” Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Isa waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.