Luka 6:48-49
Luka 6:48-49 NENO
Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”