Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 6:46-48

Luka 6:46-48 NENO

“Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? Nitawaonesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.