Luka 22:66-70
Luka 22:66-70 NENO
Kulipopambazuka, Baraza la Wazee, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, wakakutana pamoja, naye Isa akaletwa mbele yao. Wakamwambia, “Kama wewe ndiwe Al-Masihi, tuambie.” Isa akawajibu, “Hata nikiwaambia, hamtaamini. Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.” Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.”