Luka 21:27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37
Luka 21:27 NENO
Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu.
Luka 21:28 NENO
Mambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.”
Luka 21:29 NENO
Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote.
Luka 21:30 NENO
Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia.
Luka 21:31 NENO
Vivyo hivyo, mnapoyaona mambo haya yakitukia, mtambue kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
Luka 21:32 NENO
“Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia.
Luka 21:33 NENO
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Luka 21:34 NENO
“Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama mtego unasavyo.
Luka 21:35 NENO
Hivyo ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote wanaoishi katika uso wa dunia yote.
Luka 21:36 NENO
Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.”
Luka 21:37 NENO
Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni, na jioni ilipofika, alienda zake kwenye Mlima wa Mizeituni na kukaa huko usiku kucha.