Luka 21:1, 2, 3, 4
Luka 21:1 NENO
Isa alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu.
Luka 21:2 NENO
Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba.
Luka 21:3 NENO
Isa akasema, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote.
Luka 21:4 NENO
Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali yao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”