Luka 15:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10
Luka 15:1 NENO
Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Isa.
Luka 15:2 NENO
Lakini Mafarisayo na walimu wa Torati wakanung’unika wakisema, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao.”
Luka 15:4 NENO
“Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja, naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea hadi ampate?
Luka 15:6 NENO
na kwenda nyumbani. Kisha huwaita rafiki zake na majirani, na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’
Luka 15:7 NENO
Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.
Luka 15:8 NENO
“Au ikiwa mwanamke ana sarafu za fedha kumi, naye akapoteza moja, je, hawashi taa na kufagia nyumba na kuitafuta kwa bidii hadi aipate?
Luka 15:9 NENO
Baada ya kuipata, yeye huwaita rafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile sarafu yangu ya fedha iliyopotea.’
Luka 15:10 NENO
Vivyo hivyo, nawaambia, kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu juu ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”