Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 14:25-34

Luka 14:25-34 NENO

Umati mkubwa wa watu walikuwa wakisafiri pamoja na Isa, naye akageuka, akawaambia, “Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. Yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. “Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? La sivyo, baada ya kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’ “Au je, mfalme fulani akienda vita na mfalme mwingine, si yeye huketi chini kwanza na kufikiri: je, akiwa na jeshi la watu elfu kumi, ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu elfu ishirini? Ikiwa hawezi, basi yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma wajumbe na kuomba masharti ya amani. Vivyo hivyo, yeyote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. “Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, itafanywaje ili iweze kukolea tena?