Luka 14:25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34
Luka 14:25 NENO
Umati mkubwa wa watu walikuwa wakisafiri pamoja na Isa, naye akageuka, akawaambia
Luka 14:26 NENO
“Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe.
Luka 14:27 NENO
Yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Luka 14:28 NENO
“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha?
Luka 14:29 NENO
La sivyo, baada ya kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki
Luka 14:30 NENO
wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’
Luka 14:31 NENO
“Au je, mfalme fulani akienda vita na mfalme mwingine, si yeye huketi chini kwanza na kufikiri: je, akiwa na jeshi la watu elfu kumi, ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu elfu ishirini?
Luka 14:32 NENO
Ikiwa hawezi, basi yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma wajumbe na kuomba masharti ya amani.
Luka 14:33 NENO
Vivyo hivyo, yeyote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Luka 14:34 NENO
“Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, itafanywaje ili iweze kukolea tena?