Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yuda 1:1-4

Yuda 1:1-4 NENO

Yuda, mtumwa wa Isa Al-Masihi, na nduguye Yakobo. Kwa wale walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba Mwenyezi na kuhifadhiwa salama ndani ya Isa Al-Masihi. Rehema, amani na upendo ziwe kwenu kwa wingi. Wapendwa, ingawa nilikuwa ninatamani sana kuwaandikia kuhusu wokovu ambao tunaushiriki sisi sote, niliona imenipasa kuwaandikia na kuwasihi kwamba mwitetee imani iliyokabidhiwa watakatifu kwa nafasi moja itoshayo. Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri kati yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu, wanaopotosha neema ya Mungu, na kuifanya kuwa ruhusa ya kutenda maovu, wakimkana Isa Al-Masihi, ambaye pekee ni Mtawala wetu mkuu na Bwana wetu.