Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 40:15-24

Ayubu 40:15-24 NEN

“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe. Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake! Mkia wake hutikisika kama mwerezi; mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja. Mifupa yake ni bomba za shaba, maungo yake ni kama fito za chuma. Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake. Vilima humletea yeye mazao yake, nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye. Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, katika maficho ya matete kwenye matope. Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; miti mirefu karibu na kijito humzunguka. Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu; yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake. Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho, au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?