Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 8:1-7, 9-11

Yohana 8:1-7 NENO

Lakini Isa akaenda katika Mlima wa Mizeituni. Alfajiri na mapema Isa akaja tena Hekaluni; watu wote wakakusanyika, naye akaketi, akaanza kuwafundisha. Walimu wa Torati na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. Wakamwambia Isa, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, hadi wafe. Sasa wewe wasemaje?” Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Yohana 8:9-11 NENO

Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Isa akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. Isa akainuka na kumwambia, “Mwanamke, wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?” Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja, Bwana.” Isa akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako. Kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]