Yohana 8:1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 9, 10, 11
Yohana 8:2 NENO
Alfajiri na mapema Isa akaja tena Hekaluni; watu wote wakakusanyika, naye akaketi, akaanza kuwafundisha.
Yohana 8:3 NENO
Walimu wa Torati na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote.
Yohana 8:4 NENO
Wakamwambia Isa, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini.
Yohana 8:5 NENO
Katika sheria, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, hadi wafe. Sasa wewe wasemaje?”
Yohana 8:6 NENO
Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.
Yohana 8:7 NENO
Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”
Yohana 8:9 NENO
Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Isa akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake.
Yohana 8:10 NENO
Isa akainuka na kumwambia, “Mwanamke, wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?”
Yohana 8:11 NENO
Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja, Bwana.” Isa akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako. Kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]