YouVersion Logo
Search Icon

Yohana 7:45, 46, 47, 48, 49, 50, 51, 52

Yohana 7:45 NENO

Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?”

Yohana 7:46 NENO

Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.”

Yohana 7:47 NENO

Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika?

Yohana 7:48 NENO

Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini?

Yohana 7:49 NENO

Lakini umati huu wa watu wasiojua Sheria ya Musa, wamelaaniwa.”

Yohana 7:50 NENO

Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, na alikuwa mmoja wao, akauliza

Yohana 7:51 NENO

“Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”

Yohana 7:52 NENO

Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” [