Yohana 7:1, 2, 3, 4, 5, 6, 8, 9, 10
Yohana 7:1 NENO
Baada ya mambo haya, Isa alienda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi huko walitaka kumuua.
Yohana 7:3 NENO
Hivyo ndugu zake Isa wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.
Yohana 7:4 NENO
Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jioneshe kwa ulimwengu.”
Yohana 7:6 NENO
Isa akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote.
Yohana 7:8 NENO
Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.”
Yohana 7:10 NENO
Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alienda lakini kwa siri.