Yohana 6:61, 62, 63, 64, 65, 66, 67, 68, 69, 70
Yohana 6:61 NEN
Yesu alipojua kwamba wafuasi wake wananungʼunika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi?
Yohana 6:62 NEN
Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza?
Yohana 6:63 NEN
Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
Yohana 6:64 NEN
Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti.
Yohana 6:65 NEN
Akaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”
Yohana 6:66 NEN
Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.
Yohana 6:67 NEN
Hivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”
Yohana 6:68 NEN
Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Yohana 6:69 NEN
Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”
Yohana 6:70 NEN
Ndipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.”