Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 4:27-30

Yohana 4:27-30 NENO

Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au, “Kwa nini unazungumza naye?” Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini, akawaambia watu, “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Al-Masihi?” Basi wakamiminika watu kutoka mjini, wakamwendea Isa.