Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 20:24-31

Yohana 20:24-31 NENO

Lakini Tomaso (aliyeitwa Didimasi), mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Isa alipokuja. Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana Isa.” Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari, na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.” Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Isa akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.” Kisha akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.” Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!” Isa akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.” Isa alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. Lakini hii imeandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.